Maandalizi ya daftari la kudumu la wapiga kura yakamilika Mji wa Korogwe
Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa kushirikiana na maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wametoa mafunzo ya uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa wasimamizi wasaidizi pamoja na wasimamizi wa mashine za vitambulisho vya kura. Mafunzo haya yametolewa Januari 20, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Akizungumzia mafunzo haya ndugu Kasimu Kaoneka ambaye ni Afisa Elimu ya msingi na anayemuwakilisha Mkurugenzi alisema “ni muhimu kwa wote waliopata mafunzo haya kwenda na muda na kufanya kazi kwa umakini wakati wa uandikishaji”. Nae Mh. Mary Longway ambaye ni Kamishna kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) alisema “ washiriki wa mafunzo mnahitajika kuwa makini pamoja na kuzingatia maadili ya kazi yenu”.
Kwa mujibu wa ndugu Charles Mtali ambaye ni Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Mji wa Korogwe kunatarajiwa kuwa na vituo sabini na sita (76) vya uandikishaji, huku zoezi la uandikishaji litaanza Januari 23 hadi 29 mwaka huu. Vituo vitafunguliwa saa mbili (2) asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili (12) jioni.
Kwa upande mwingine Bwana Petro Ryioba ambaye ni msimamizi wa mashine za vitambulisho vya kura alisema kuwa mafunzo ni mazuri sababu wawezeshaji wamejitahidi kutoa elimu ya ya kutosha namna ya kutumia mashine za vitambulisho. Vilevile Bi. Shangwe Msuya ambaye pia ni mshiriki wa mafuzo haya alisema mafunzo waliyotolewa na wawezeshaji yameeleweka vizuri hivyo anaimani kubwa washiriki watafanya kazi ya uandikishaji kwa ufanisi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.