Madiwani wa Mji wa Korogwe wapitia taarifa ya hesabu 2021/22
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mhe. Francis Komba ameongoza Baraza la Madiwani ambalo ni maalumu kwaajili ya kupitia Taarifa za Hesabu katika mwaka wa fedha 2021/22 kabla ya kuwasilishwa kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali. Baraza hilo la Madiwani lilihudhuriwa pia na Wataalamu wa Halmashauri pamoja na Wawakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga limefanyika Septemba 29, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
“Natoa pongezi kwa Wataalamu wote wa fedha kwa kufanya kazi kwa bidii iliyopelelea kuandaa taarifa nzuri ya hesabu” alisema Mhe. Fancis Komba ambae ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakati wa upitiaji wa Taarifa za Hesabu katika Baraza la Madiwani. Mhe. Komba alifafanua kuwa ni vyema Wataalamu wote wa fedha katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe wafanye kazi kwa weledi huku wakizingatia kanuni na taratibu zote za fedha ili kuiwezesha Halmashauri kupata hati safi.
“Wataalamu wa fedha msijisahau kwa kuandaa taarifa nzuri ya hesabu, kazi bado inaendelea na kipindi kijacho msije mkajisahau mkaanguka” alisema Ndugu Sebastian Masanja ambaye ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga wakati wa Baraza la Madiwani. Nae Ndugu Valentine Christopher ambaye ni Kaimu Mkuurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe alitoa shukrani kwa Madiwani pamoja na Wawakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwa kupitia Taarifa ya hesabu pamoja na kuipitisha ili iweze kuwasilishwa katika hatua nyengine.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.