Madiwani watakiwa kuunga mkono jitihada za ukusanyaji wa mapato
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. William Mwakilema amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kuunga mkono jitihada za ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri. Jitihada hizo ni pamoja na kushirikiana na Wataalamu wa Halmashauri katika kubuni vyanzo vipya vya mapato pamoja na kuendeleza vile vilivyopo. Mhe. Mwakilema alitoa kauli hiyo wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani linachohitimisha kipindi ya Robo ya Kwanza katika mwaka wa fedha 2024/2025. Baraza hilo lilifanyika Novemba 12, Mwaka huu (2024) katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
“Madiwani kwa kushirikiana na Wataalamu wa Halmashauri jitahidini kubuni vyanzo vipya vya mapato” alisema Mhe. William Mwakilema ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe. Mhe. Mwakilema alifafanua kuwa Halmashauri ikifanikisha kukusanya fedha za kutosha kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato, fedha hizo zitasaidia katika uendeshaji wa Halmshauri pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Nae Mhe. Nassoro Mohamed ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mji wa Korogwe kwaniaba ya Madiwani alisema “Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya shukrani kwa kutukumbusha, Madiwani tuko tayari kushirikiana na Wataalamu wa Halmashauri katika kubuni vyanzo vipya pamoja na kusimamia vilivyopo kwa ukamilifu”.
Kwa upande mwengine, Bi. Mwashabani Mrope ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe alisema “Swala la ukusanyaji wa mapato ni letu wote, Madiwani, Mkurugenzi pamoja na Wataalamu wa Halmashauri. Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya tunakushukuru kwa kutusisitiza tuweze kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa mapato”. Bi. Mwashabani alifafanua kuwa Halmashauri kwa kushirikiana na Madiwani tayari imeshaanza utekeleaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo (Soko la Manundu) ambayo itasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.