Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetekeleza Miradi ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu na Afya katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Miradi iliyotekelezwa ni mingi sana katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe ikiwemo ya Elimu, Afya na Barabara. Kwa upande wa Elimu na Afya miradi mikubwa imekamilika na huduma zinaendelea kutolewa. Miradi hiyo ni Ujenzi wa Shule ya Sekondari Majengo iliyojengwa kata ya Majengo uliogharimu Shilingi Milioni 584,280,029.00, Ujenzi wa Shule ya Sekondari Msambiazi kata ya Mtonga uliogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 584,280,028,.00 na Ujenzi wa Zahanati ya Lwengera Darajani uliogharimu Shilingi Milioni 32,080,000.00 umejengwa katika kata ya Old Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.