Mama Samia awafuta machozi Wananchi wa Old Korogwe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewafuta machozi Wananchi wa Kata ya Old Korogwe iliyopo katika Mji wa Korogwe baada ya kuwapatia fedha kiasi cha Shilingi Milioni Themanini kwaajili ya Ujenzi wa Vyumba Vinne vya Madarasa katika Shule ya Msingi Old Korogwe. Wananchi hao walikuwa na kilio cha muda mrefu kuhusu uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo baada ya baadhi ya vyumba kutotumika kutokana na ukongwe wa shule hiyo iliyojengwa tokea enzi za ukoloni.
Baada ya kukabidhiwa fedha hizo Kiasi cha Shilingi Milioni Themanini, Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Kwazomolo kwa kushirikiana na Wataalamu wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe walianza utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Vinne vya Madarsa. Hadi kufikia Mei 13, Mwaka huu (2024) Mradi huo wa Ujenzi ulishafikia hatua ya Msingi pamoja na ujazaji wa vifusi ili kuanza upandishaji wa kuta.
Akizungumzia utekelezaji wa Mradi huo baada ya kuutembelea na kuona utekelezaji wake, Bi. Mwashabani Mrope ambaye ni Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Korogwe alisema “Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni msikivu kwa Wananchi wake. Tayari ameshatupatia fedha kwaajili ya utekelezaji wa Mradi, ni vyema Wananchi na Halmashauri tukashirikiana kwa pamoja katika kufanikisha Mradi huu”.
“Mama Samia ametufanya Wananchi wa Old Korogwe kuwa na furaha tele baada ya kutuletea Mradi wa ujenzi, tulisahaulika kwa muda mrefu sasa ni wakati wetu kutembea vifua mbele” alisema Bw. Peter Mhina ambaye ni Mwananchi kutoka Kata ya Old Korogwe. Bw. Mhina alisissitiza kuwa Wananchi wa Old Korogwe wanaunga mkono jitihada za Rais katika kufanikisha uboreshaji Elimu hapa nchini. Utelelezaji wa Mradi wa Ujenzi katika Shule ya Msingi Old korogwe ulianza Mwezi Mei, 2024 na unatarajiwa kukamilika Mwezi Juni, 2024.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.