Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini atembelea miradi ya maendeleo
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mhe. Dkt. Alfred Kimea akiambatana pamoja na Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe ametembelea miradi ya Ujenzi wa Vituo vya Afya inayotekelezwa kwa fedha za tozo za miamala ya simu pamoja na miradi ya Ujenzi wa Madarasa inayotekelezwa kwa Fedha za Uviko 19. Ukaguzi huo wa miradi ya maendeleo umefanyika January 22, mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe.
Ziara ya Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini pamoja na Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe ilitembelea Mradi wa Ujenzi wa Madarasa katika Shule ya Sekondari Nyerere Memorial iliyopo Kata ya Manundu. Miradi mingine ni Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mgombezi kilichopo Kata ya Mgombezi pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kwamsisi kilichopo Kata ya Kwamsisi.
“Natoa pongezi kwa uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa Madarasa” alisema Mhe. Dkt. Alfred Kimea wakati akikagua Mradi wa Ujenzi wa Madarasa Matatu katika Shule ya Sekondari ya Nyerere Memorial. Mhe. Dkt. Kimea alifafanua kuwa ni vyema fedha zilizoelekezwa kwenye miradi husika zikakamilisha miradi kwa wakati ili miradi hiyo iweze kuwanufaisha walengwa waliokusudiwa.
“Natoa shukrani kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali” alisema Mhe. Francis Komba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Diwani wa Kata ya Mtonga wakati wa ziara ya ukaguzi wa Miradi ya maendeleo. Mhe. Komba alifafanua kuwa ili miradi ya maendeleo iweze kudumu kwa muda mrefu ni vyema jamii inayozunguka mradi husika iweze kushirikishwa katika ujenzi ili wawe sehemu ya ulinzi wa maradi wao.
Nae Bw. Mohamed Amri ambaye ni Mwananchi wa Kata ya Mgombenzi na pia ni Katibu wa Ujenzi wa Mradi wa Kituo cha Afya cha Mgombezi alitoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mhe. Dkt. Alfred Kimea na Kamati nzima ya Fedha ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa kututembelea ujenzi wa miradi ya maendeleo ili kuona jinsi miradi hiyo ilivyotekelezwa.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.