Mchakato wa baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Korogwe kuhamia Mji wa Korogwe waiva, Halmashauri zote mbili zaafikiana
Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe zimekutana kujadili namna ya kukabidhiana baadhi ya maeneo ya kiutawala kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kwenda Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Halmashauri hizo zimekutana katika kikao maalumu cha baraza la ushauri wa kisheria katika Wilaya ya Korogwe. Kikao hicho kilifanyika Januari 17, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Akizungumzia mchakato huu Mh. Kissagwakisa Kasongwa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe alisema kuwa mchakato huu umetokana na kuhama kwa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kwenda eneo la Kwasunga katika kutekeleza agizo la Mh. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na agizo la Mh. Selemani Jafo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Wajumbe wa Halmashauri zote mbili walitoa baraka zao kuridhia mchakato huu hivyo kuendelea kwa ngazi ya Mkoa na hatua nyinginezo. Maeneo yaliyopendekezwa kuhamia Halmashauri ya Mji wa Korogwe ni Kata zote zilizopo Tarafa ya Korogwe na Magoma ambazo ziko kumi (10), Vijiji arobaini na moja (41) pamoja na Vitongoji miambili na tano (205). Lengo kuu la kuhamisha maeneo haya Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kwenda Halmashauri ya Mji wa Korogwe ni kuwawezesha wanachi wa maeneo haya kupata huduma za kijamii kwa haraka.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.