Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mh. Francis Komba akiambatana na Madiwani wa kamati ya Fedha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope Pamoja na Wataalamu wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe katika ziara ya kutembelea Miradi ya Maendeleo. Mh. Komba amewataka Wataalamu kuwa wazalendo na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali. Kauli hiyo aliitoa katika ziara ya Madiwani wa kamati ya Fedha na Utawala kama sehemu ya kuhitimisha Robo ya Tatu katika Mwaka wa Fedha 2024/ 2025. Ziara hiyo ilifanyika Aprili 28 Mwaka huu (2025) katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe.
Miradi iliyotembelewa na na Mh. Komba pamoja na kamati ya Fedha na Utawala ni Mradi wa ujenzi wa chumba cha Tehama kilichopo Shule ya Msingi Mbeza katika kata ya Manundu, Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Mganga mbili kwa moja (Two in one) katika Zahanati ya Lwengera Darajani inayopatikana kata ya Old Korogwe, Ukarabati wa Soko la Samaki lililopo kata ya Manundu, Mradi mwingine uliotembelewa ni Ujenzi wa Mradi wa Nyumba ya Mwalimu Mbili kwa moja (Two in One) pamoja na Maendeleo ya Shule ya Sekondari Msambiazi iliyopo kata ya Mtonga na Mradi wa Mwisho kutembelewa ulikuwa ni Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi katika Shule ya Sekondari Ngombezi inayopatikana kata ya Mgombezi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.