Mkuu wa Wilaya ya Korogwe (DC) Mh. William Mwakilema akiambatana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe (DAS) Bi. Mwanaidi Rajab ametembelea Banda la Halmashauri ya Mji wa Korogwe katika Maonesho ya Nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea Mkoani Morogoro kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Manispaa ya Morogoro. Mh.Mwakilema amewataka Wataalamu wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kusimamia uzalishaji wa Wanyama wenye sifa na wenye ubora ili kuweza kushindana na Soko la Nje ya Tanzania hata la Kidunia . Mh. Mwakilema alitoa kauli hiyo wakati akitembelea Banda la Halmashauri ya Mji wa Korogwe Agosti 6, 2025 Manispaa ya Morogoro.
Aidha Mh. Mwakilema alipongeza Banda la Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa ubunifu na Maandalizi mazuri katika Maonesho hayo. Mh. Mwakilema aliishukuru Idara ya Afya kupitia Wataalamu wake kwa kutoa Huduma nzuri kwa Wananchi wanaokuja kupata matibabu Katika Banda la Mji wa Korogwe. Mh. Mwakilema alipata wasaa wa kupima uzito, Sukari na Presha katika Banda la Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Kauli mbiu ya Nanenane Mwaka huu inasema” Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.