Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Bi. Zahara Msangi akiambatana na Wakuu wa Idara na Vitengo watembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ikiwa ni utaratibu wa kila wiki katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Ziara hiyo imefanyika Novemba 20, 2025 katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe.
Bi. Zahara Msangi amewataka wasimamizi wa miradi hiyo kusimamia miradi hiyo ili kuhakikisha inamalizika kwa wakati na katika ubora unaohitajika. Mkurugenzi huyo ametoa onyo kali kwa yoyote atakaekiuka taratibu na sheria katika kutekeleza majukumu yake katika usimamizi wa miradi inayoendelea.
Aidha Bi. Zahara Msangi amewaomba wasimamizi wa miradi hiyo kuidhinisha malipo ya wazabuni kwa wakati bila kutoa visingizio. Katika kusema hayo amewataka mafundi katika mradi kufanya kazi kwa bidii na uweledi kwa maslahi ya kujenga Taifa bora.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa madarasa 2 ya mfano na matundu 6 ya vyoo, Madarasa 3 ya msingi na matundu 6 ya vyoo ya msingi katika Kituo shikizi cha Kitifu, umaliziaji wa chumba 1 cha darasa Matondoro, ujenzi wa madarasa 2 na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Antakaye, ujenzi wa madarasa 3 na matundu 6 ya vyoo ya elimu msingi katika shule ya msngi Mbeza Mazoezi, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na ofisi, umaliziaji wa vyumba 2 vya madarasa, umaliziaji wa chumba 1 cha darasa katika shule ya msingi New Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.