Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Bi. Zahara Msangi amewataka Waalimu na Watendaji wa Kata kuhakikisha Miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao inatekelezwa kwa kuzingatia taratibu na miongozo ya utekelezaji wa miradi hiyo. Kufuata miongozo kutawezesha miradi hiyo kukamilika kwa ubora na kwa wakati.
Bi Zahara Msangi ameyasema hayo katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa miradi kilichofanyika Novemba 22, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Korogwe.
Kikao cha tathmini ya utekelezaji wa miradi kilihusisha Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu, Watendaji Kata na Mitaa pamoja na Wenyeviti wa Kamati za Miradi. Wengine walioshiriki ni Idara ya Ujenzi, Mipango, Kitengo cha Fedha, Manunuzi na Wakuu wa Idara zenye Miradi inayotekelezwa na Halmashauri.
Bi. Zahara Msangi amewataka watumishi kufanya kazi kwa upendo na ushirikiano ili kuwezesha Halmashauri kufikia malengo yake.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.