Mji wa Korogwe waadhimisha Siku ya Mazingira Duniani
Juni 5 ya kila mwaka Halmashauri ya Mji wa Korogwe huungana na Taasisi mbalimbali hapa Nchini na Dunia kwa ujumla kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, lengo likiwa ni kuelimishana na kusisitiza umuhimu wa kutunza mazingira ili kunufaisha kizazi kilichopo na cha badae.
Katika Mji wa Korogwe shughuli mbalimbali zinazohusiana na Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani zilianza kufanyika kuanzia Juni 1 hadi 5, mwaka huu ambayo ndio siku ya kilele cha Maadhimisho ya haya. Hapa Nchini kaulimbiu ya mwaka huu ni “Tutunze Mazingira: Tukabiliane na Mabadiliko ya Tabianchi” Kauli ambayo inasisitiza wananchi kutunza mazingira ili kukabiliana na athari mbalimbali zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumzia Siku ya Mazingira Duniani, Ndugu Mohammed Mndeme ambaye ni Kaimu Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe alisema “katika maadhimisho ya mwaka huu wataamu wa mazingira tumewatembelea wadau mbalimbali wa mazingira kwa lengo la kuelimishana namna ya kuhifadhi mazingira ili yawe endelevu kwa vizazi vijavyo”. Ndugu Mndeme alitoa ushauri wa wananchi kwa kusema “kazi ya uhifadhi wa mazingira sio jukumu la Serikali pekeyake bali ni jukumu la Wananchi wote kuhakikisha mazingira yanaimarishwa vyema”.
Nae Ndugu Juma Mhina ambaye ni mdau wa uhifadhi wa mazingira kutoka Kijiji cha Kwamsisi alitoa shukrani kwa Idara ya Mazingira kwa jitihada inayofanya katika kutoka elimu kwa wadau wa mazingira na wananchi kwa ujumla kuhusu utunzaji wa mazingira. Ndugu Mhina pia alitoa nasaha kwa vijana kwa kusema " vijana wachangamkie fursa ya uhifadhi wa mazingira katika kujiajiri kwenye biashara ya utengenezaji wa vitalu vya miti ya mbao, matunda pamoja na maua ili kujikwamua kiuchumi".
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.