Mji wa Korogwe waadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
Wanawake wa Mji wa Korogwe wameungana na wanawake wote Duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Maadhimisho ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Tarehe 8 Mwezi Machi. Maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika katika Mtaa wa Kwasemangube uliopo Kata ya Magunga. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Wanawake katika uongozi chachu kufikia Dunia yenye usawa”.
Maashimisho ya siku ya wanawake Duniani kwa mwaka 2021 ni muendelezo wa harakati za wanawake wa Mji wa Korogwe kukutana kwenye jukwaa moja wakiwa na malengo mbalimbali kama vile kupeana faraja, kuelimishaana pamoja na kupeana mbinu mbalimbali za kufungua milango ya fursa katika Nyanja za Kiuchumi, Kisiasa pamoja na Kijamii.
“natoa pongezi kwa wanawake wa Mji wa Korogwe kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani” alisema Mhe. Kissa Kasongwa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe na ndiye mgeni rasmi. Katika maadhimisho hayo Mhe. Kasongwa alisisitiza kuwa ili wanawake waweze kupata maendeleo ni vyema wafanye kazi kwa bidii. Nae Mhe. Iddi Kabwele ambaye ni Diwani wa Kata ya Magunga alisema “Wakinababa pia tunatoa pongezi kwa Wanawake katika maadhimisho haya ya Siku ya Wanawake Duniani”.
“Natoa pongezi kwa vikundi vyote vya Wakinamama ambao wamerudisha mkopo wa Halmashauri kwa wakati” alisema Dr. Fortunata Silayo ambaye ni Afisa Mifugo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe anayemwakilisha Mkurugenzi katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Dr. Silayo alilfafanua kuwa Halmashauri itaendeleza harakati zake katika kuwapatia mikopo wanawake ili waweze kujikomboa kiuchumi.
Nae Bi. Charity Sichona ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii alisema “wanawake tujitokeze kwenye Ofisi za Ustawi wa Jamii ili kufichua ukatili wa kijinsia” Bi. Charity alifafanua kuwa katika jamii kuna wanawake wengi ambao hufanyiwa ukatili wa kijinsia hivyo ni muda muafaka kujitokeza katika idara husika ili waweze kupata msada katika kukabiliana na changamoto hizo. Kwaupande mwengine, Wanawake waliojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani walitoa shukrani kwa Serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Wanaharakati mbalimbali wa maswala ya Wanawake kwa kufanikisha maadhimisho hayo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.