Mji wa Korogwe wajipanga kupambana na majanga
Halmashauri ya Mji wa Korogwe umejipanga kupambana na majanga ya moto na mengine ya asili katika idara zake ili kujiepusha na uharibifu wa mali za umma pamoja na vifo vya watu. Mikakati hii imewekwa Oktoba 23, mwaka huu katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe baada ya kupata mafunzo ya kupambana na moto pamoja na uokoaji kwa ujumla katika maeneo ya kazi yaliyotolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Akizungumzia mafunzo hayo ndugu Sharifu Salehe afisa habari kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kituo cha Korogwe alisema ni muhimu taasisi kupanga mikakati ya kupambana na moto pamoja uokoaji katika majanga mbalimbali kabla ya majanga ya moto kujitokeza na kuleta madhara katika idara za serikali. Ndugu salehe alifafanua zaidi ni vyema taasisi ya seikali kuweka mikakati imara ya uokoaji ili kujiepusha za uharibifu wa mali ya umma pamoja na vifo vya watu
Nae ndugu Ramadhani Sekija afisa kilimo wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe anayemuwakilisha Mkurugenzi ameshukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kutoa mafunzo ya kupambana na moto pamoja na uokoaji kwa ujumla kwa wakuu wa vitengo na idara katika halmashauri. Ndugu sekija aliendelea kusema kuwa elimu waliyoipata itasaidia kuweka mikakati imara katika kupambanana na moto pamoja na majanga mengine katika idara za serikali hususani idara za Afya pamoja na Elimu.
Kwa upande mwingine Mh. Nasoro Hassani ambaye ni diwani wa kata ya Kwamsisi alisema mafunzo ya kupambana na moto pamoja na majanga mengine yametolewa katika muda muafaka wakati Mji wa Korogwe unakumba na majanga ya moto pamoja na majanga mengine ya asili. Mh. Hassani ametolea wito madiwani wote waliopata mafunzo kuwa mabalozi katika kata zao na kuwasisitiza wananchi kuwa na vifaa vya kuzimia moto ambapo kwa sasa wananchi wengi wanatumia majiko ya gesi.
Akihitimisha kutoa mafunzo ndugu Zubeda Bakari ambaye ni afisa ukaguzi kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji alitoa ushauri kwa wakuu wa vitengo, idara pamoja na waheshimiwa madiwani ni vyema majengo ya serikali pamoja na wanachi kabla ya kujengwa kupeleka ramani za majengo katika Jeshi la zimamoto na uokoaji. Lengo la ukaguzi wa huu ni kuhakikisha ramani ya nyumba pamoja na mtaa ni inarahisisha uokoaji panapotokea majanga ya moto na mengine ya asili.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.