Mji wa Korogwe wapanga kutumia Shilingi Bilioni 26 Mwaka 2023/24
Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wamepitisha Bajeti ya Shilingi Bilioni 26 {26,323,677,000} kwa ajili ya matumizi ya Halmshauri hiyo katika mwaka wa fedha 2023/24. Bajeti hiyo ya Halmashauri ilipitishwa wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya Pili katika Mwaka wa Fedha 2022/23 kilichofanyika Februari 09, Mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauriya Mji wa Korogwe.
“Nitoe pongezi kwa Mkurugenzi pamoja na Wataalamu wote wa Halmashauri kwa maandalizi mazuri ya Bajeti ya Mwaka wa fedha 2023/24”. Alisema Mhe. Francis Komba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Mhe. Komba alisistiza kuwa Madiwani wote watasimama imara kuhakikisha Bajeti ya Mwaka wa fedha 2023/24 itatekelezeka kwa lengo la kuwanufaisha Wananchi wa Mji wa Korogwe.
“Mpango huu wa Bajeti ya Mwaka wa fedha 2023/24 unalenga kuwashirikisha Wananchi katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini”. Alisema Bw. Elinlaa Kivaya ambaye ni Mchumi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Bw. Kivaya alifafanua kuwa Mpango huo wa Bajeti ya Mwaka wa fedha 2023/24 umeandaliwa kwa kushirikisha Wananchi kuanzia ngazi ya Vijiji, Mtaa hadi Kata.
Kwa upande mwengine, Wananchi wa Mji wa Korogwe pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walioshiriki katika Baraza la Madiwani la Robo ya Pili katika mwaka wa Fedha 2022/23 walitoa pongezi kwa Mkurugenzi na Halmashauri kwa ujumla kwa maandalizi mazuri ya Bajeti inayolenga kuwakwamua Wananchi kiuchumi na kupunguza umaskini.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.