Mji wa Korogwe wapokea msaada wa vifaa vya michezo
Halmashauri ya Mji wa Korogwe imepokea Msaada wa Mipira Nane (8) kwaajili ya Michezo mbalimbali katika Shule za Msingi na Sekondari. Mipira hiyo ilitolewa na Mdau wa Michezo Bw. Ally Lugendo ambaye ni Afisa Utamaduni wa Jiji la Dar es Salaam. Baada ya kupokelewa kwa Mipira hiyo, Bi. Minaeli Mjema ambaye ni Afisa Utamaduni wa Mji wa Korogwe Agosti 22, Mwaka huu (2024) aliwakabidhi Walimu wa Michezo kutoka Shule mbalimbali kwa ajili uendelezaji wa Sekta ya Michezo. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Jengo la Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.