Mji wa Korogwe washinda tuzo ya elimu kwa mwaka 2019
Halmashauri ya Mji wa Korogwe imepata tuzo ya usimamizi bora wa mtihani wa kidato cha sita mwaka 2019 kwa mkoa wa Tanga. Tuzo ambayo hutolewa kila mwaka nchini Tanzania ili kuwatambua na kuwaunga mkono wataalamu wa elimu.. Tuzo hii ilitolewa Oktoba 26, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City uliopo katika eneo la Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Akizungumzia tuzo hii Bi. Gilda Mashuda ambaye ni Afisa Takwimu Idara ya Sekondari katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe alisema tuzo hii iliandaliwa na taasisi ya Global Education Link kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Baraza la Mitihani Tanzania. Alifafanua kuwa Halmashauri ya Mji wa Korogwe imepata tuzo kupitia Mwl. Theresia Kawele anayefundisha shule ya Sekondari Old Korogwe ambaye alishiriki katika usimamizi wa mtihani wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana ya Korogwe
Nae Mwl. Theresia Kawele anayefundisha shule ya Sekondari Old Korogwe ambaye ni mshindi wa tuzo ya usimamizi ubora wa mitihani kwa mkoa wa Tanga alisema anafuraha kubwa kutangazwa mshindi wa tuzo hii kwani tuzo imeipa heshima kubwa shule ya sekondari Old Korogwe, Halmashauri ya Mji wa Korogwe na mkoa wa Tanga kwa ujumla. Mwl. Kawele alifafanua zaidi kuwa anaimani kubwa ushindi wake umetokana na kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuzingatia taratibu za usimamizi wa mitihani hivyo taasisi husika kumpa tuzo ya cheti pamoja na ngao
Kwa upande mwingine mwl. Ally Sengasu anayefundisha shule ya Old Korogwe alisema anafuraha kubwa kuona tuzo ya ubora wa elimu kwa mkoa wa Tanga imechukuliwa na mwl. Theresia Kawele anayefundisha shule ya Sekondari Old Korogwe. Mwl. Sengasu alisema tuzo hii imeipa heshima kubwa shule yao na kutoa motisha kwa walimu kufanya kazi kwa bidii.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.