Mji wa Korogwe watakiwa kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mji wa Korogwe Mhe. Francis Komba ameitaka Halmshauri ya Mji wa Korogwe kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ili iweze kufikia lengo iliyojiwekea. Kauli hiyo aliitoa wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani kinachohitimisha kipindi cha Robo ya Tatu katika Mwaka wa fedha 2023 / 2024. Kikao hicho kilifanyika Mei 07, Mwaka huu katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Mpaka kufikia Aprili 30, Mwaka huu (2024) Halmashauri ya Mji wa Korogwe imeshakusanya Mapato kwa Asilimis 79. Mapato hayo yamekusanywa kutoka vyanzo mbalimbali vya Mapato vilivyopo Halmshauri huku ikibakiza Asilimia 21 ya ukusanyaji wa Mapato ili kufikia lengo iliyojiwekea katika Mwaka wa fedha 2023 / 2024.
“Kila Mtaalamu wa Halmashauri kwa nafasi yake aongeze kasi ya ukusanyaji wa mapato ili tufikie lengo tulilojiwekea” alisema Mhe. Francis Komba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani. Mhe. Komba alisisitiza kuwa kuongezeka kwa mapato katika Halmashauri kutasaidia Halmashauri kuwa na fedha za kutosha zitakazosaidia katika utekelezaji wa Miradi ya Mendeleo.
“Mheshimiwa Mwenyekiti Maelekezo yote uliyotupa tumeyapokea na tutayafanyia kazi” alisema Bw. Elinlaa Kivaya ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani. Bw. Kivaya alifafanua kuwa Halmashauri imejipanga vyema katika kuhakikisha inakamilisha Asilimia 21ya mapato ilizobakia ili kufikia lengo iliyojiwekea katika Mwaka wa fedha 2023 / 2024.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.