Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe akabidhi pikipiki 32 kwa wataalamu wa kilimo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope amekabidhi pikipiki 32 aina ya Hero (Hunter) kwa Wataalamu wa Idara ya Kilimo. Pikipiki hizo 32 walizokabidhiwa Wataalamu wa Idara ya Kilimo zilitolewa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi hapa Nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika Oktoba 23, Mwaka huu (2024) katika Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
“Natoa shukrani za dhati kwa Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia pikipiki 32 kwa ajili ya Wataalamu wa Idara ya Kilimo katika Halmashauri yetu” alisema Bi. Mwashabani Mrope ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Kwaupande mwengine, Bi. Mwashabani amewaasa Wataalamu wa Idara ya Kilimo kuzitunza vyema pikipiki walizokabidhiwa pamoja na kuzitumia katika matumizi sahihi ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.
Nae Bw. Ramadhani Sekija ambaye ni Mkuu wa Idara ya Kilimo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe alisema “Kwa niaba ya Wataalamu wa Idara ya Kilimo, natoa shukrani za dhati kwako Mkurugenzi kwa kutukabidhi pikipiki, Pikipiki hizi zitaturahisishia usafiri wakati wa kutimiza majukumu yetu”.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.