Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe akabidhi vifaa vya michezo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope amekabidhi vifaa vya michezo pamoja na fedha kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Korogwe Bw. David Ngwilizi kwaajili ya maandalizi ya Ligi ya Post Uchaguzi Cup. Ligi ya Post Uchaguzi Cup, ni Ligi maalumu kwaajili ya kuwashukuru Wananchi wa Wilaya ya Korogwe kwa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwa Amani na Utulivu. Makabidhiano hayo yalifanyika Desemba 6, 2024 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Ligi ya Post Uchaguzi Cup itakayoshirikisha Timu 16 kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe inatarajiwa kuanza Desemba 7, Mwaka huu (2024) Saa Tisa na Nusu (Alasiri) katika Kiwanja cha Magereza kilichopo Mtaa wa Memba katika Mji wa Korogwe. Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Ligi hiyo atakuwa Bi. Mwashabani Mrope ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.