Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe akagua Ujenzi wa Miradi Sekta ya Elimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope akiambatana Pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hiyo amefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Ujenzi katika Sekta ya Elimu yenye thamani ya Shilingi Milioni Mia Nne Sabini na Mbili na Laki Tano. Miradi hiyo ya Ujenzi, inahusisha Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa pamoja na Matundu ya Vyoo katika Shule za Msingi Pamoja na Sekondari. Ziara hiyo ya ukaguzi wa Miradi ilifanyika Mei 02, Mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe.
Miradi ya Ujenzi katika Sekta ya Elimu inayotekelezwa katika Mji wa Korogwe, inatekelezwa na fedha kutoka Serikali Kuu pamoja na fedha za Wahisani katika Mradi wa EP4R kupitia Serikali Kuu. Utekelezaji huo wa Miradi, unahusisha Ujenzi wa Vyumba 08 vya Madarasa katika Shule za Msingi pamoja na Vyumba 08 vya Madarasa katika Shule za Sekondari. Ujenzi wa Vyumba vya madarasa unaendana pamoja na Ujenzi wa Matundu 42 ya Vyoo katika Shule za Msingi Pamoja na Matundu 16 ya Vyoo katika Shule za Sekondari.
Miradi yote ya Ujenzi katika Sekta ya Elimu inayotekelezwa katika Mji wa Korogwe, Utekelezaji wake ulianzia Aprili 06, Mwaka huu na inatarajiwa ifikapo June 30, Mwaka huu Miradi yote iwe imekamilika.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.