Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope akiambatana na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe ametembelea Eneo lililopendekezwa kwa ajili ya Matumizi ya Dampo. Ziara hiyo ilifanyika Agosti 26, 2025 katika kata ya Old Korogwe. Bi. Mwashabani Mrope alimwaagiza Mkuu wa Idara ya Ardhi kusitisha kutoa kibali cha ujenzi kwa Mwananchi yeyote kujenga Eneo hilo pia aliendelea kusema kuwa “Wananchi waliokwisha kujenga Nyumba zao wasiondolewe bali warasimishwe.”
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.