Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe atembelea kiwanda cha matofali
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Happy Luteganya akiambatana pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo ametembelea kiwanda cha uzalishaji wa matofali ya saruji kinachomilikiwa na Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Lengo la kutembelea kiwanda hicho ni kuangalia namna matofali yanavyozalishwa kwaajili ya matumizi ya ujenzi wa makazi pamoja na miradi ya maendeleo. Kiwanda hicho ambacho ni miongoni mwa vyanzo vya mapato ya Halmashauri kinazalisha matofali yenye ubora ya inchi tano na inchi sita yanayouzwa kwa bei nafuu pamoja na pevisi kwaajili ya matumizi mbalimbali. Ziara hiyo ilifanyika Desemba 12, Mwaka huu (2024) katika Kata ya Bagamoyo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.