Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Zahara Msangi akiambatana na wataalamu wa mapato pamoja na wataalamu wa biashara ametembelea vyanzo mbalimbali vya mapato vinavyopatikana katika Stendi ya John Kijazi.Ziara hiyo ilifanyika Novemba 4, 2025 katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe. Katika ziara hiyo Mkurugenzi alitembelea jumla ya maduka 143 vilevile alipata wasaa wa kutembelea na kuona mtambo unaozalisha matofali ya saruji.
Kwa upande mwingine Bi. Zahara Msangi alikutana na wafanyabiasha mbalimbali pamoja na mawakala wa usafirishaji katika Stendi ya Kijazi na kutoa kero zao mbele ya Mkurugenzi.Naye Wakala wa basi la Osaka Bw. Omary Musa alimuomba Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe kudhibiti mabasi yote yanayopakia abiria na kushusha abiria nje ya Stendi ya Balozi John Kijazi ili kuweza kuongeza mapato zaidi ya Halmashauri. Aidha Bw. Justine Elias mfanyabiashara katika Stendi ya John Kijazi amemuomba Mkurugenzi wa Mji kuwa changamoto kubwa wanayokutana nayo kwenye biashara zao ni kuwepo kwa vituo vingi nje ya Stendi ya John Kijazi na kusababisha abiria wengi kutoingia ndani ya Stendi hiyo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.