Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe atoa mahitaji katika vituo vya kulelea watoto
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bw. Burhan Ngulungu akiambatana pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo ametembelea Kituo cha kulelea Watoto yatima cha Zubeiriyah kilichopo Kata ya Kwamndolwa pamoja na Kituo cha Watoto wenye uhitaji maalumu cha Kilimani kilichopo Kata ya Mtonga katika Mji wa Korogwe. Lengo la kutembelea vituo hivyo ni kuwajulia hali Watoto pamoja na kuwapatia mahitaji katika msimu huu wa sikukuu ya mwaka mpya 2025. Ziara hiyo ilifanyika Desemba 30, 2024.
Mahitaji yaliyokabidhiwa kwa Watoto yatima pamoja na wenye uhitaji maalumu ni pamoja na mchele, unga wa sembe, maharage, sukari, biskuti, juisi, majani ya chai, sabuni pamoja na mafuta ya kupikia.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.