Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh.Dkt. Balozi Batilda Burian akiambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mh. William Mwakilema, Katibu tawala wa Wilaya ya Korogwe (DAS) Bi. Mwanaidi Rajabu, Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope pamoja na Wataalamu wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya Daktari inayojengwa kwenye Zahanati ya Lwengera iliyopo kata ya Old Korogwe ili kuona hatua iliyofikia ya ujenzi huo. Ziara hiyo ya kutembela mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Daktari imefanyika Mei 27, Mwaka huu (2025) katika Zahanati ya Lwengera Halmashauri ya Mji wa Korogwe
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.