Mkuu wa Wilaya ya Korogwe afungua semina ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mh. Kissagwakisa Kasongwa amefungua semina ya mawakala wa vyama vya siasa pamoja na waandikishaji wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu. Ufunguzi huu wa semina umefanyika Oktoba 7, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Akizungumzia mchakato wa uchaguzi Mh. Kasongwa amewataka mawakala wa vyama vya siasa pamoja na waandikishaji wa uchaguzi kufanya kazi kwa weledi ili kuepukana na changamoto zinazoweza kujitokeza. Aliendelea kusema kuwa uaminifu na nidhamu katika zoezi zima la uchaguzi ni jambo la msingi.
Katika semina hii mkuu wa wilaya aliambatana pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya Korogwe akiwemo mkuu wa jeshi la Polisi, Uhamiaji na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Kamati ya ulinzi na usalama ilisisitiza kuwa ni muhimu mawakala wa vyama vya siasa na waandikishaji wa uchaguzi kuzingatia kanuni na sheria za uchaguzi ili uchaguzi ukamilike kwa amani.
Kwa upande mwingine ndugu Albert Nyan’ali hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo ya Korogwe aliwaapisha mawakala pamoja na waandikishaji wa uchaguzi wa serikali za mitaa ili kufanya kazi kwa uadilifu.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.