Mkuu wa Wilaya ya Korogwe ahamasisha uwekezaji katika sekta ya utalii
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Basilla Mwanukuzi amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji ya Mji wa Korogwe kutenga Bajeti ya kutosha kwaajili ya uhamasishaji wa uwekezaji wa sekta ya utalii katika Mji wa Korogwe. Maagizo hayo aliyatoa wakati wa Kikao cha Kamati cha Ushauri wa Wilaya (DCC) kilichofanyika Januari 25, mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
“Tutenge Bajeti ya kutosha katika uhamasishaji wa utalii ili tuendane na sera ya uwekezaji hapa nchini” alisema Mhe. Basilla Mwanukuzi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe wakati akipokea Taarifa ya Makadirio ya Bajeti ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa Mwaka wa Fedha 2022/23. Mhe. Basilla alifafanua kuwa iwaopo Halmashuri itahamasisha uwekezaji katika sekata ya utalii, utalii utasaidia kuchangia mapato ya kutosha katika halmashauri.
“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya maelekezo yote uliyoyatoa tumeyapokea na tutayafanyia kazi” alisema Ndugu Nicodemus Bei ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Ndugu Bei alifafanua kuwa Halmashauri ya Mji wa Korogwe imejipanga vyema katika kuhakikisha inaongeza mapato ya Halmashauri kwa Mwaka wa Fedha 2022/23.
Kwa upande mwengine, Bw. Jumanne Semagongo ambaye ni Afisa Habari wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe alifafanua kuwa Mji wa Korogwe umebahatika kuwa lango kuu la kuelekea Mikoa ya Kanda ya Kaskazini na kua kituo kikubwa na cha mapunziko ya wageni wakisubiri kuendelea na safari zao. Pia Mji wa Korogwe umebarikiwa kuwa na utajiri mkubwa wa vivutio vya utalii. Vivutio hivyo vya utalii vinajumuisha Utalii wa Kimazingira, Utalii wa Kihistoria pamoja na Utalii wa Kiutamaduni unaosadifu maisha halisi ya Wananchi wa Mji wa Korogwe.
Kuhusu Taarifa ya Makadirio ya Bajeti ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa Mwaka wa Fedha 2022/23, Bw. Juma Mhina ambaye ni Mwananchi wa Mji wa Korogwe na Kiongozi wa Dini aliyeshiiriki katika kikao cha Kamati ya Ushauri wa Wilaya alisema “natoa pongezi kwa Mkrurugenzi wa Halmashauri na watalamu wote kwa ujumla kwa kuandaa makadirio mazuri ya Bajeti” Bw. Mhina alifafanua kuwa Bajeti ya Halmashauri katika Mwaka wa Fedha 2022/23 ni nzuri na imeakisi uhitaji halisi wa Wananchi wa Mji wa Korogwe”.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.