Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mh. William Mwakilema amewataka Watendaji wa Kata kutoka Halmashauri mbili ya Korogwe Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe,Wakuu wa Idara na Vitengo kufuata misingi ya Utawala Bora na Kuimarisha Demokrasia ya kweli hapa Nchini Kwa Kulinda Haki za Binadamu Pamoja na kufuata Maadili na miiko ya uongozi. Lengo kuu ya Mafunzo hayo ya Uraia na Utawala Bora kwa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ni kuwajengea Viongozi uwezo kuhusu Haki na Uwajibikaji kwa kufuata Katiba ya Nchi .Mh. Mwakilema ameyasema hayo wakati akifungua Mafunzo ya Uraia na Utawala Bora kwa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Machi 22, (2025) Mwaka huu katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.