MNEC Paul Makonda atimiza ahadi yake ya kutoa Kiti cha Umeme
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Korogwe Mjini Mhe. Thobias Nungu (Nyakusagira) kwa niaba ya MNEC Paul Makonda amekabidhi Kiti cha Umeme kwa ajili ya Mtu Mwenye uhitaji maalumu. Kiti hicho cha Umeme chenye thamani ya Shilingi Milioni Tano kilikabidhiwa kwa Bw. Yohana Kihiyo ambaye ni Balozi wa Nyumba Kumi, Shina Namba Tatu katika Mtaa wa Magunga. Makabidhiano hayo yalifanyika Januari 24, Mwaka huu katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Korogwe Mjini iliyopo Mtaa wa Majengo.
Wakati ya Ziara ya MNEC Paul Makonda Januari 21, Mwaka huu katika Wilaya ya Korogwe ikiwa ni miongoni mwa Ziara ya Umarishaji wa Chama cha Mapinduzi pamoja na Kuzungumza na Wananchi hapa Nchini. MNEC Paul Makonda alitoa ahadi ya kumsaidia Bw. Yohana Kihiyo Mtu mwenye uhitaji maalumu wa Kiti ili kiweze kumsaidi kutoka eneo moja hadi jingine wakati akitekeleza majukumu yake ya kila siku. Mbali na Kiti cha Umeme MNEC Paul Makonda Pia alimpatia Bw. Yohana Kihiyo Shilingi Milioni Moja kwaajili ya huduma ya Bima ya Afya.
“Uongozi wa CCM Wilaya ya Korogwe Mjini pamoja na Korogwe Vijijini tunatoa shukrani zetu za dhati kwa MNEC Paul Makonda kwa kumpatia Kiti cha Umeme Bw. Yohana Kihiyo, kiti hiki cha Umeme kitaweza kumrahisishia usafiri wakati akitekeleza majukumu yake.” Alisema Mhe Thobias Nungu (Nyakusagira) ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Korogwe Mjini. Mhe Nungu alisisitiza kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea na utaratibu wa kusikiliza kero za Wananchi na kuzipatia ufumbuzi wa kudumu.
Natoa shukrani kwa MNEC Paul Makonda pamoja Uongozi Mzima wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Korogwe Mjini kwa kunikabidhi Kiti cha Umeme, kiti hichi kitanirahisishia usafiri katika kazi zangu”. Alisema Bw. Yohana Kihiyo ambaye ni mnufaika wa Kiti cha Umeme. Bw. Kihiyo pia alitoa shurani za dhati kwa Bw. Tito Mganwa ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa kumuunga mkono mpaka hatua aliyofikia.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.