Halmashauri ya Mji wa Korogwe imekamilisha Ujenzi wa Vyumba Vitatu (03) vya Madarasa na Matundu Sita ya Vyoo katika Shule ya Msingi Kwakombo iliyopo kata ya Kwamsisi. Mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi Milioni Themanini na Nane na Lakini Sita (88,600,000.00).
Kiasi hicho cha Fedha kimehusisha Ujenzi wa Vyumba Vitatu vya Madarasa, Matundu Sita ya Vyoo Pamoja na ununuzi wa Madawati Arobaini na Tano. Kila Darasa moja limepata mgao wa Madawati Kumi na tano, Kila Dawati moja linakaliwa na Wanafunzi Watatu. Fedha zote za Mradi zilitolewa na Serikali kuu kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Awali na Msingi hapa Nchini (BOOST) kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.