Mratibu wa Mikopo ya Asilimia kumi (10%) Halmashauri ya Mji wa Korogwe B. Blandina Mhina afunga Mafunzo yaliyokuwa yanaendelea kwa muda wa siku tatu kwa Vikundi Tisa vilivyoidhinishiwa kupatiwa mikopo ya Asilimia kumi kwa kuwataka Washiriki wa Mafunzo hayo kusimamia fedha hizo kwa lengo lililokusudiwa ili waweze kujiinua kiuchumi. Bi. Blandina Mhina alitoa kauli hiyo wakati wa kufunga Mafunzo kwa Vikundi 9 vilivyoidhinishiwa kupewa Mikopo ya Asilimia kumi na Idadi ya Washiriki waliohudhuria mafunzo yapata Arobaini na tano. Mafunzo hayo yamefungwa Mei 06 mwaka huu (2025) katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Wawezeshaji wa Mafunzo hayo kwa Siku ya mwisho ni Wataalamu mbalimbali Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.