Mratibu wa Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Tanga Bw. Ramadhani Ally akiambatana na Waratibu wa Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoani,Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe Bi. Mwanaidi Rajabu, Bi. Mwashabani Mrope Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wilaya, Pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe amefanya ziara ya kutembelea miradi na njia itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025. Ziara hiyo imefanyika katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe Aprili 08, 2025.
Katika ziara hiyo ya Mratibu wa Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Tanga Bw. Ramadhani Ally amesisitiza suala la Uzalendo na Uwajibikaji katika miradi ya Serikali kwa kufuata kanuni na Sheria za Manunuzi kwa kutumia Mfumo wa Manunuzi ( NesT). Miradi iliyotembelewa na Waratibu wa Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Tanga ni Pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya Mganga katika Zahanati ya Lwengera Darajani iliyopo kata ya Old Korogwe, Mradi wa Kikundi cha Vijana uliopo kata ya Majengo.
Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Masuguru iliyopo kata Masuguru,Ukarabati wa Vibanda 38 katika Soko kuu la Manundu vinavyopatikana katika kata ya Manundu, Mradi wa Ujenzi wa Chujio la Maji linalojengwa katika Mtaa wa Kwamkole uliopo kata ya Mtonga, na Mradi wa Mwisho ni Mradi wa Nyumba ya Mwalimu (Two in One) iliyopo Mtaa wa Msambiazi katika Kata ya Mtonga.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.