Kitakwimu Halmashauri ya mji wa Korogwe ina jumla ya shule za msingi 29 za serekali ambapo kuna upungufu wa vyumba vya madarasa 124, na ofisi za waalimu 45; hadi sasa jumla ya vyumba vya madarasa 83 na ofisi ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi kila shule.
Hata hivyo leo tarehe 02/01/2019 wananchi wa kata ya Mtonga wamejumuika pamoja katika zoezi la msaragambo uliofanyika shule za msingi Msambiazi na Kwamkole. Wakiongozwa na diwani wao mhe. Komba pamoja na viongozi wengine wa serekali za mtaa huo, wamewasaidia mafundi kazi za kubeba maji,kokoto,zege, na mawe kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitano na ofisi 3.
Licha ya hiyo,ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe imeunga mkono jitihada za wananchi kwa kutoa mchango wa fedha na wataalam ambapo hadi sasa imeshachangia jumla ya shilingi 11,545,000 kwa miradi yote miwili na inaendelea kushirikiana na wananchi katika kila hatua.Pia kuna michango kutoka vyanzo vingine kama vile mfuko wa jimbo jumla 960,000, guvu za jamii jumla 1,900,000, harambee jumla 5,23000 na michango ya wananchi wenyewe jumla 1,753,500 zote kwa pamoja zikifika 16,681,500.
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mhula wa masomo kuanza, Halmashauri ya mji wa Korogwe inatarajia kuwa na ongezeko la wanafunzi watakaojiunga na elimu ya msingi kutokana na hamasa kubwa ya elimu bila malipo inayotolewa chini ya serekali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dr. John Pombe Magufuli.Hivyo jitihada zote hizi lengo ni kuwawezesha watoto wote waliofika umri wa kwenda shule kupata sehemu ya kusomea kwa maana ya madarasa.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.