Mwakilema: Tujenge utamaduni wa kusafisha maeneo yetu
Kuelekea kilele cha Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, Mwaka huu. Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. William Mwakilema amewanasihi Wananchi wa Wilaya ya Korogwe kujenga Utamaduni wa kusafisha maeneo yanayowazunguka bila kusukumwa na Serikali. Nasaha hiyo aliitoa Aprili 24, Mwaka huu wakati wa zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika katika Kituo cha Afya cha Majengo kilichopo Kata ya Majengo Mjini Korogwe.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. William Mwakilema ameshiriki zoezi la usafi wa mazingira katika Kituo cha Afya cha Majengo ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Katika zoezi hilo la usafi wa mazingira Mhe. Mwakilema aliambatana Pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe Bi. Mwanaidi Rajabu, Maafisa Tarafa wa Tarafa zilizopo Wilaya ya Korogwe, Wataalamu mbalimbali wa Serikali Pamoja na Wananchi.
Kauli Mbiu ya Sherehe za Miaka 60 ya Muungano: Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa letu”
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.