Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bw. Burhan Ngulungu ambaye Amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mh. William Mwakilema amewataka wanaoendesha Mashirika yasiyo ya Kiserikali kufuata Sheria za Nchi husika na miongozo inayotolewa na Serikali wakati wanapotekeleza Miradi ya Maendeleo. Bw. Ngulungu alitoa kauli hiyo kwenye Ufunguzi wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Serikali. Ufunguzi huo umefanyika Julai 01, 2025 Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Siku ya Jumanne.
Naye Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Bw. Joseph Gweba alieleza kuwa lengo la kikao hicho cha Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali ni kuwapitisha Wajumbe katika kuwasilisha na Kujadili mchango wa NGOs kwa Mwaka 2024.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.