Mwenge wa Uhuru wafungua Miradi ya Shilingi Bilioni 1.4 katika Mji wa Korogwe
Kiongozi wa Mbio za Mwnge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2022, Sahili Geraruma amekagua na kufungua Miradi ya Maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.4 katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Miradi hiyo iliyofunguliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa inajumuisha Miradi ya Elimu, Afya, Maji, Ufugaji wa Kuku, Ujenzi wa Barabara pamoja na Mradi wa Vijana wa Bodaboda. Mwenge wa Uhuru uliwasili katika Mji wa Korogwe na Kupokelewa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kalist Lazaro Juni 5, Mwaka huu ukitokea Wilaya ya Lushoto.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru Mwaka 2022 ni “Sensa ni msingi wa mipango ya maendeleo: Shiriki kuhesabiwa, tuyafikie maendeleo ya Taifa.
“Miradi ya maendeleo ni mizuri na nimeifungua” alisema Sahili Geraruma ambaye ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2022. Ndugu Geraruma alisisitiza kuwa ili Serikali iweze kufikia maelengo yake katika ujenzi wa miradi ya maendeleo, Wasimamizi wa Miradi hiyo wanatakiwa kufanya kazi kwa ufanisi ili kuhakikisha Miradi inakamilika bila ya changamoto zozote. Katika hatua nyengine Sahili Geraruma aliwataka Wananchi wote waweze kushiriki katika Sensa ya Mwaka 2022 kwa maendeleo ya Nchi yetu.
“Viongozi na Wananchi wote kwa ujumla tuna furaha kubwa kwa kutufungulia miradi yetu katika Mji wa Korogwe” alisema Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kalist Lazaro wakati wa ufunguzi wa miradi ya maendeleo. Mhe. Lazaro alifafanua kuwa ushauri wote uliotolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wameupokea na wataufanyiwa kazi ili kuhakikisha wanaopewa dhamana ya usimamamizi wa miradi wanafanya kazi kwa ufanisi.
Kwa upande mwengine, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Dkt. Alfred Kimea alitoa shukrani kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha mbalimbali katika Mji wa Korogwe kwaajili ya ujenzi wa Miradi ya Maendeleo. Dkt Kimea alisema “Natoa shukrani kwa Mama Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kunipatia fedha kwa ajiili ya kukamilisha miradi ya Maendeleo katika Mji wa Korogwe”.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.