Akitembelea miradi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita,kiongozi wa mbio za mwenge 2018 Ndugu Charles Kabeho alijionea miradi hiyo na kusema kuwa miradi iliyozinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi inapaswa kukamilika ndani ya muda uliokusudiwa ili kuondoa kero wanazopata wananchi wa Korogwe.Pia alifurahishwa na kikundi cha wajasiria mali kinachojihusisha na utengenezaji wa viatu cha (Vijana Shoes Production) na kuwataka vijana wote kuiga mfano huo ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira na kusadifu sera ya uchumi wa viwanda.
Mbio za mwenge wa uhuru 2018 katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe ulikimbizwa na kupitia miradi (6) kwa kuiwekea mawe ya msingi miradi 2, kufungua miradi 2 na kukagua miradi 2.Miradi yote ina thamani ya shilingi 2,286,502,796 kwa mchanganuo ufuatao:-
SEREKALI KUU
|
2,038,727,792
|
HALMASHAURI YA MJI
|
8,822,000
|
MCHANGO WA WANANCHI
|
36,300,000
|
WADAU WA MAENDELEO
|
202,653,004
|
JUMLA
|
2,286,502,796
|
Miradi iliyohusika katika mbio hizo ni pamoja na ujenzi wa kituo cha afya cha Majengo kitakachogharimu jumla ya shilingi 50,200,0000, ujenzi miundo mbinu ya maji Msambiazi jumla shilingi 629,064,434 ujenzi wa jengo la madarasa shule ya msingi Kilole jumla ya shilingi 102,422,000, uboreshaji wa barabara ya Manundu jumla ya shilingi 843,063,358.Pia kuna miradi ya vikundi vya wajasiriamali wadogo chini ya Idara ya maendeleo ya jamii ambavyo ni pamoja na kikundi cha Vijana ushonaji wa viatu cha majengo shilingi 4,300,000 na kikundi cha watengeneza mikate cha (Yagaza bakeri na Snacks Manundu) shilingi 202,653,004.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.