Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Balozi Dkt. Batilda Burian akabidhiwa Mwenge wa Uhuru pamoja na wakimbiza Mwenge Sita (6) wa kitaifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Daresalaam Mh. Albert Chalamila. Makabidhiano hayo yamefanyika Juni 6, 2025 katika Uwanja wa Ndege wa Tanga kata ya Mwanzange Jijini Tanga. Mwenge ukiwa Mkoani Tanga utakimbizwa katika Halmashauri 11 na utazindua miradi ya Maendeleo, Utaweka jiwe la Msingi na kutembelea miradi yote yenye gharama ya Shilingi Bilioni 28.6. Mwenge wa Uhuru utapokelewa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Juni 9, 2025 ukitokea Halmashauri ya Mji Handeni na kukabidhiwa Halmashauri ya Bumbuli Juni 10,2025.
Kauli mbiu ya mwaka huu wa Mwenge wa Uhuru 2025 inasema “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.