Mwenyekiti, Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe watembelea miradi ya elimu na afya
Mwnyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mhe. Francis Komba akiambatana na Mkurugenzi pamoja na Kamati ya Fedha na Utawala ya Halamshauri hiyo wametembelea miradi ya afya na elimu ikiwa ni hatua ya ukaguzi wa miradi katika kuhitimisha kipindi cha Robo ya Tatu katika mwaka wa Fedha 2021/22. Ziara hiyo ya kutembelea miradi katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe imefanyika Aprili 27, mwaka huu.
Katika zira hiyo, Kamati ya Fedha na Utawala walitembelea mradi wa Ujenzi wa jengo la Wagojwa wa Dharura katika Hospitali ya Mji wa Korogwe (Magunga ) wenye thamani ya Shilingi Milioni Mia Tatu, Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kwamsisi wenye thamani ya Shilingi Milioni Miambili na Hamsini pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Bagamoyo wenye thamani ya Shilingi Milioni Mia Nne.
Pamoja na kutembelea miradi ya elimu na afya, Kamati ya Fedha na Utawala pia ilitembelea Miradi mingine ukiwepo Mradi wa Karakana ya Sevia wenye thamani ya Shilingi Milioni Sita, Mradi huo wa Karakana ya Sevia unaomilikiwa na Vijana ambao wanaojishughulisha na ufundi wa magari. Mradi mwengine ni ufungaji wa Kamera za CCTV katika Kituo cha Mabasi cha Balozi John Kijazi wenye thamani ya Shilingi Milioni Tano.
“Mhandisi wa Halmashauri hakikisha ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa dharura linakua na ubora wa hali ya juu na kukidhi vigezo vyote kwa mujibu wa ramani uliyopewa” alisema Mhe. Francis Komba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Diwani wa Kata ya Mtonga wakati akifanya ukaguzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharura katika Hospitali ya Mji wa Korogwe (Magunga). Mhe. Francis Komba alisisitiza kuwa Wakandarasi wote waliopewa ujenzi wa miradi ya Halmashauri wahakikishe wanakamilisha miradi yote ndani ya muda uliopangwa.
“Halmashauri imejipanga vyema kuhakikisha kila Mkandarasi aliyepewa kandarasi ya ujenzi anatimiza majukumu yake kwa ufanisi, Mkandarasi yoyote atakayekabidhi jengo lenye mapungufu hatomaliziwa fedha zake mpaka arekebishe mapungufu yaliyojitokeza katika jengo lake” alisema Bi. Bernadetha ambaye ni Mchumi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe anayemuwakilisha Mkurugenzi. Bi. Bernadetha alisisitiza kuwa Mkandarasi yoyote atakayejihisi analegalega katika kutimiza majukumu yake ni vyema akajisalimisha mapema kwa maslahi ya Halmashauri na Serikali kwa ujumla.
“ Wananchi wa Mji wa Korogwe tuanatoa shukrani kwa Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Serikali kwa ujumla kwa kufanikisha mradi wa Ujenzi wa Jengo la Wagojwa wa Dharura katika Hospitali ya Mji wa Korogwe (Magunga), Jengo litakapokamilika litasaidi kutoa matibabu ya dharura kwa Wananchi wa Mji Korogwe na maeneo ya jirani” alisema Bw. Juma Stambuli ambaye ni Mwananchi wa Kata ya Magunga katika Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.