Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Tanga Bw. Abdulrahman Shiloow amewata Wataalamu kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Tanga kusimamia na kuitunza Miradi inayotekelezwa na Serikali kwani Serikali imetumia Fedha nyingi katika kukamilisha Ujenzi huo. Kauli hiyo aliitoa kwenye Kikao cha Wajumbe wa ALAT mkoa kabla ya kuanza kutembelea Miradi ya Maendeleo. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Ziara hiyo ilifanyika Machi 28, Mwaka huu (2025) katika maeneo mabalimbali ya Mji wa Korogwe.
Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Tanga akiambatana na Makamu Mwenyekiti, Katibu wa ALAT mkoa , Waheshimiwa wenyekiti wa Halmashauri za Mkoa wa Tanaga,Wakurugenzi wote kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Tanaga Pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo.Miradi iliyotembelewa na Timu ya ALAT Mkoa wa Tanga ni Pamoja na Ujenzi wa Vyumba vitatu vya Madarasa na Matundu Sita ya Vyoo katika Shule ya Msigi Kwakombo iliyopo kata ya Kwamsisi,Zahanati ya Lwengera iliyopo kata ya Old Korogwe,Mradi wa Kikundi cha Vijana kilichopo kata ya Majengo,Mradi wa Maji wa Miji 28, Ujenzi wa Vyumba vitatu vya Madarasa na Matundu Nane ya Vyoo katika Shule ya Sekondari Semkiwa.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.