Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Mh. Rajabu Abdallah ambaye ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa akiambatana na Halamshauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga, pamoja na Halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi Mji wa Korogwe,Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mh. William Mwakilema, Mbuge wa Korogwe Mjini Dkt.Alfred Kimea, Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope,akikagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Ziara hiyo ya kutembelea miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe imefanyika Mei 16, mwaka huu (2025). Kwa upande mwingine Mh. Rajabu Abdallah alichangia Magunia kumi (10) ya mchele yenye thamani ya Shilingi Milioni mbili na nusu (2,500,000 kwaajili ya chakula cha Wanafunzi wanaokaa Bweni katika Shule ya Sekondari ya Ngombezi.
Miradi iliyotembelewa na Mh. Rajabu Abdalla Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi katika Shule ya Sekondari Ngombezi iliyoko Kata ya Mgombezi na Chumba cha maabara ya Sayansi katika Shule ya Sekonadari New Bagamoyo iliyopo kata ya Bagamoyo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.