Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mh. Thobias Nungu,katibu wa Chama cha Mapinduzi Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mh. Evarest Mluge, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe akiambatana pamoja na kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Waheshimiwa Madiwani wametembelea Ujenzi wa miradi ya maendeleo ili kujionea utekelezaji wa miradi hiyo. Kwaupande mwingine Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mh. Nungu ametoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope kwa usimamizi mzuri wa fedha za miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Mh. Mwenyekiti alitoa pongezi hizo kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Korogwe Mjini iliyofanyika Mei 15, 2025.
MIradi iliyotembelewa na kamati ya Siasa ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe ni pamoja na Ujenzi wa chujio la maji linalojengwa Mtaa wa kwamkole kata ya Mtonga, Ukarabati wa ujenzi wa vibanda soko la Samaki Manundu,Mradi wa Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Majengo, na Mradi wa mwisho ni ujenzi wa Nyumba ya Mganga mfawidhi Zahanati ya Lwengera iliopo kata ya Old Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.