Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe atembelea Miradi ya Maendeleo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mhe. Francis Komba akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala, pamoja na Wataalamu wa Halmashauri ametembelea na kufanya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kwa lengo la kuangalia Utekelezaji wa Miradi hiyo na hatua iliyofikia ili iweze kuwahudumia Wananchi. Ziara hiyo imefanyika kwa Siku Mbili kuanzia Agosti 17 hadi 18, Mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe ikiwa ni hatua za kuhitimisha ukaguzi wa Miradi katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2022/ 23.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Miradi ya Ujenzi wa Shule Mpya, Madarasa, Nyumba za Walimu pamoja na Ununuzi wa Vitanda vya Wanafunzi. Miradi mingine ni Ujenzi wa Vituo vya Afya, Zahanati pamoja na Ununuzi wa Vifaa vya Matibabu. Pia Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala walitembelea Mradi wa Kikundi cha Walemavu pamoja na Eneo la Uwekezaji la Wamachinga. Miradi yote iliyotembelewa inatekelezwa kupita Fedha za Serikali Kuu, Fedha za Wahisani kupitia Serikali Kuu pamoja na Fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri.
“Natoa Shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia Fedha za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Mji wa Korogwe” alisema Mhe. Francis Komba amabye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakati wa ukaguzi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kwamsisi pamoja na Vifaa vya Matibabu katika Kituo hicho. Mhe. Komba alifafanua kuwa Miradi yote ya Afya pamoja na Elimu itakapokamilika itasaidia kuchagiza maendeleo kwa Wananchi wa Mji wa Korogwe.
Katika hatua nyengie, Mhe. Francis Komba alitoa pongezi kwa Mkurugenzi pamoja na Wataalamu wote. Mhe. Komba alisema, “Natoa pongezi kwa Mkurugenzi pamoja na Wataalamu wote wa Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa Miradi ya Elimu, Miradi hii inang’arisha Mji wetu wa Korogwe”. Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bw. Tito Mganwa alitoa Shukurani kwa Mwenyekiti pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala kwa kutembelea Miradi ya Maendeleo na kujionea utekelezaji wa Miradi hiyo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.