Mwenyekiti wa Mji wa Korogwe ahimiza ukusanyaji wa mapato
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mhe. Francis Komba amemtaka Mkurugenzi na Wataalamu wote wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo mbalimbali ili Halmashauri iweze kupata fedha za kutosha zitakazoiwezesha Halmashauri kuwahudumia Wananchi kwa ufanisi.
Mhe. Francis Komba alitoa maagizo hayo wakati wa Baraza la Madiwani la Kawaida lililofanyika Mei 06, mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Katika Baraza hilo Madiwani walikutana pamoja kwaajili ya kuwasilisha Taarifa mbalimbali za maendeleo katika Kata zao ikiwa ni hatua ya kuhitimisha kipindi cha Robo ya Tatu katika Mwaka wa Fedha 2021/22.
“Mkurugenzi na Wataalamu wote, hakikisheni mnaongeza kasi ya ukusanyaji wa mapatao ili Halmashauri iweze kupata fedha za kutosha zitakazosaidi kuwahudumia Wananchi kwa ufanisi” alisema Mhe. Francis Komba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Diwani wa Kata ya Mtonga. Mhe. Komba alisisitiaza kuwa kila Mtaalamu wa Halmashauri kwa nafasi yake ahakikishe anashiriki ipasavyo katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
“Mheshimiwa Mwnyekiti maagizo yote uliyotupatia tumeyapokea na tutayafanyia kazi” alisema Bi.Charity Sichona ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe anayemuwakilisha Mkurugenzi. Bi.Charity alifafanua kuwa Halmashauri imejipanga vyema katika kuhakikisha inaelekeza nguvu zote katika ukusanyaji wa mapato ili Halmashauri iweze kuwa na fedha za kutosha zitakazosaidia kuwahudumia Wananchi.
Katika hatua nyengine, Madiwani wameipongeza Halmashauri jinsi inavyojitahidi katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu na afya ikiwa ni jitihada za kuwapatia huduma Wananchi jirani na maeneo yao. “naipongeza Halmashauri kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Mji wa Korogwe (Magunga)” alisema Mhe. Iddi Kabwele ambaye ni Diwani wa Kata ya Magunga.
“Nampongeza mwenyekiti kwa kuwahimiza Wataalamu wa Halmashauri kuongeza bidii katika ukusanyaji wa mapato, Halmashauri ikiwa na mapato ya kutosha itaweza kutatua matatizo ya Wananchi kwa haraka” alisema Bw. Abdulimajid Shemahonge ambaye ni Mwananchi wa Mji wa Korogwe aliyeshiriki katika Baraza la Madiwani la Kawaida linalohitimisha Robo ya Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2021/22.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.