Mwenyekiti wa Mji wa Korogwe atembelea Miradi ya Maendeleo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mhe. Francis Komba akiambatana na Madiwani wa Kamati ya Fedha, Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe Bw. Buruhan Ngulungu pamoja na Wataalamu wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe ametembelea Miradi ya Maendeleo ili kuona hatua liyofikia. Ziara hiyo ya kutembelea Miradi ya Maendeleo ilifanyika Julai 29, Mwaka huu (2024) katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe.
Ziara ya kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Mji wa Korogwe ilifanyika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji katika kuhitimisha Baraza la Madiwani katika kipindi cha Robo ya Nne katika Mwaka wa Fedha 2023 / 2024. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Mradi wa Upanuzi wa Dampo katika eneo la Bagamoyo, Mradi wa Ujenzi wa Matundu ya Vyoo vya Kisasa katika Shule za Msingi Bagamoyo, pamoja na Mradi wa Kuchakata Maji Taka katika eneo la Bagamoyo.
Mradi mwengine ni Kikundi cha Ufugaji Nyuki katika Mtaa wa Majengo, Mradi wa Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Nyerere, Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Kituo cha Mafunzo ya Walimu (Teachers Resource Centre) katika Mtaa wa Masuguru, Mradi wa Ujenzi wa Kisima cha Maji Safi katika Mtaa wa Makwei uliotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), pamoja na Mradi wa Kiwanda cha Matofali ya Saruji katika eneo la Bagamoyo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.