Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Bw. Ismail Ali Ussi ameweka Jiwe la Msingi Nyumba ya Mganga Mfawidhi Lwengera Darajani katika Halmshauri ya Mji wa Korogwe. Kukamilika kwa Nyumba hii ya Mganga Mfawidhi itasaidia kutoa Huduma kwa haraka na kwa wakati. Hapo mwanzo Watumishi walikuwa wanakaa mbali na kituo cha kazi kusababisha wananchi kuchelewa kupata huduma. Mradi unategemea kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni Tisini na Nane (98,000,000.) mpaka kukamilika kwake ikiwa Milioni 93,220,000 ni mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Milioni 4,780,000 ikiwa ni nguvu za Wananchi.
Ussi ameyasema hayo Juni 9, 2025 baada ya kuweka jiwe la Msingi kwenye Nyumba ya Mganga Mfawidhi katika Zahanati ya Lwengera darajani iliyopo kata ya Old Korogwe Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Mwenge wa Uhuru 2025 katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe ulitembelea miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Kikundi cha Umoja wa Vijana (Kimawaba) Kata ya Majengo, Ukarabati wa Vibanda katika Soko la Samaki kata ya Manundu, Nyumba ya kuishi Familia mbili ya Walimu wa Shule ya Sekondari ya msambiazi kata ya Mtonga (Two in One), Mradi wa Visima vya Maji kata ya Mgombezi, na Mradi wa Kito cha Mafuta cha Afroil Investment LTD kata ya Majengo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.