Mkutano huo uliitishwa na NHIF(bima ya afya),mwishoni mwa wiki hii na kufanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa korogwe.Washiriki wa mkutano walikua ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Reuben Shigela,Katibu tawala Eng. Zena A. Said pamoja na wakurugenzi na Wakuu wa wilaya zote za Tanga,Mwenyekiti Halmashauri ya mji wa Korogwe,waganga wakuu wa Halmashauri na waratibu wa NHIF katika kila Halmashauri na timu ya maafisa kutoka NHIF ikiongozwa na mkurugenzi mkuu wa NHIF.
Aidha lengo kuu la mkutano huu lilikua kujadili utekelezazi na uboreshaji wa mradi wa mama na mtoto unaofadhiliwa na Ujerumani.Mradi huu unawawezesha mama wajawazito wote Tanzania kujifungulia hosipitalini pasipo kuchajiwa gharama yoyote.Ufadhili huu unalenga kuondoa vifo vya mama na mtoto vilivyokua vinatokana na kinamama kujifungulia majumbani kwa kukwepa gharama za hosipitali.Ni dhahiri kwamba mama akijifungulia hosipitalini yupo mikono salama kutokana na matatizo mbalimbali yanayojitokeza katika uzazi ambapo atapata msaada wa wataalam wenye weledi.
Hata hivyo kikao hiki kiliweka ufahamu wa pamoja ya kua mama anapokwenda kujifungulia kwenye vituo vya afya,mhudumu anayemhudumia anapaswa kumwandikisha katika kadi maalumu ambapo itatumwa NHIF ili kituo kirudishiwe gharama alizotumia mama huyo.Afisa kutoka NHIF alieleza kuwa mojawapo ya sababu zinazofanya kituo au hosipitali kutopata fedha hizo ni kushindwa kutuma taarifa za uzazi au kuchelewa kuziwasilisha kwa wakati.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.