Mji wa Korogwe wapata Milioni 35.7 kwajili ya Ujenzi wa Matundu ya Vyoo
Halmshauri ya Mji wa Korogwe imepokea Kiasi cha Shilingi Milioni Thelasini na Tano na Laki Saba Kutoka Serikalini kwaajili ya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Matundu ya Vyoo katika Shule za Msingi zilizopo katika Halmashauri hiyo. Mradi huo unatarajiwa kunufaisha Shule za Msingi takribani Nne na tayari utekelezaji wake umeshaanza tokea Mwezi Mei, 2024 na unatarajiwa kukamilika Mwezi Juni, 2024.
Shule ninazotarajiwa kunufaika na Mradi huo ni Pamoja na Shule ya Msingi Matondoro, Kwakombo, Msambiazi Pamoja na Bagamoyo. Kukamilika kwa Mradi huo wa Ujenzi wa Matundu ya Vyoo katika shule hizo kutasaidia kupunguza uhaba wa Matundu ya Vyoo na kufanya Shule hizo kuwa na mazingira rafiki kwa Wanafunzi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.