Halmashauri ya Mji wa Korogwe yakabidhi hundi ya mkopo wenye thamani ya Shilingi Milioni Sitini (60,000,000) kwa vikundi Tisa (09) vya Wanawake , Vijana na Watu wenye ulemavu.Mkopo huo usio na riba unatokana na mapato ya ndani ya Asilimia kumi ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe.Mkopo wa wa awamu ya pili umetolewa Mei 20,2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.Mgeni rasmi katika utoaji wa mkopo huo alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mh. Francis Komba. Halmashauri ya Mji wa Korogwe imejipanga kutoa Mkopo wa Asilimia kumi kwa awamu Nne Mfululizo katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.